Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya Sabaya kuendelea leo

8b9fd063b405716369580e4bef12fd3d Kesi ya Sabaya kuendelea leo

Mon, 14 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kesi ya uhujumu uchumi, utakatishaji fedha haramu na kumiliki genge la uhalifu inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya (35) na wenzake sita itaendelea leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha.

Kesi hiyo iliahirishwa wiki iliyopita kutokana na Hakimu, Patricia Kisinda anayeisikiliza kupata udhuru.

Hakimu Pamela Meela alihairisha kesi hiyo na kuwataka mawakili wa pande zote wajipange ili leo iweze kuendelea.

Kabla ya kuhairishwa kwa kesi hiyo, Wakili Edmund Ngemela alikuwa akiendelea kumwongoza shahidi wa tano, Jackson Macha (30) ambaye ni mshitakiwa wa sita katika kesi hiyo.

Washitakiwa wengine ni, Enock Mnkeni (41), Watson Mwahomange (27), John Aweyo (45), Syliverster Nyegu (26), Jackson Macha (29) na Nathan Msuya (31).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live