Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya Sabaya Yapigwa Kalenda

Sabaya?fit=1000%2C562&ssl=1 Lengai Ole Sabaya, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai

Fri, 13 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shauri la Uhujumu Uchumi namba 27 la mwaka 2021 linalomkabili aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita limetajwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha huku upande wa Jamhuri ukieleza upelelezi wa shauri hilo umekamilika.

Upande wa Jamuhuri, ukiongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali, Tumaini Kweka ameiambia Mahakama Mbele ya Hakimu mkazi mfawidhi, Martha Maumbuga, tayari upelelezi umekamilika nakuiomba mahakama kuwapa tarehe nyingine ili waweze kukamisha taratibu nyingine za kisheria, ndipo Hakimu Mkazi Mfawidhi, Martha Maumbuga akaahirisha kesi hiyo mpaka tarehe 27 Agosti kwa ajili ya kusomwa.

Sabaya na wenzake wamerudishwa tena rumande hadi tarehe tajwa itakapofika watarudishwa kwaajili ya usikilizwaji wa kesi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live