Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya Sabaya: Uamuzi mdogo kutolewa leo

Sabaya?fit=1000%2C562&ssl=1 Kesi ya Sabaya: Uamuzi mdogo kutolewa leo

Mon, 23 Aug 2021 Chanzo: Nipashe

​​​​​​​MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, leo inatarajia kutoa uamuzi mdogo wa kukubali au kukataa maelezo yanayodaiwa kuandikwa kituo cha polisi na shahidi wa pili wa utetezi Silvester Nyegu (26), kutumiwa na Wakili wa Serikali kumhoji shahidi huyo.

Silvester Nyegu (26), Daniel Mbura na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya, wanakabiliwa na kesi ya jinai namba 105 yenye mashtaka matatu ya unyang’anyi wa kutumia silaha.

Agosti 20, mwaka huu hakimu mwandamizi wa mahakama hiyo, Odira aliahirisha kusikiliza kesi hiyo baada ya mawakili wa utetezi kupinga uhalali wa wakili wa Jamhuri kumhoji shahidi huyo kupitia maelezo yanayodaiwa aliandika kituo cha polisi.

Awali kabla ya kuahirishwa kwa shauri hilo, kulitokea mvutano wa kisheria kwa mawakili wa pande zote mbili hali iliyomlazimu hakimu kuahirisha kesi kwa dakika 15 kwenda kupitia hoja za mawakili hao.

Hakimu mwandamizi wa mahakama hiyo, alidai mahakamani kwamba baada ya kupitia hoja hizo, na kufanya uchunguzi wake hakufikia mwisho kwa kuwa jambo hilo halikuwa dogo kama mawakili hao walivyodhani.

“Katika kupekuwa na kupitia hoja zenu nimeona kuna maswali mengi yamejitokeza, hivyo tunaahirisha kusikiliza shauri hili hadi Agosti 23, mwaka huu nitatoa uamuzi mdogo kwa kuwa pande zote zipo kwa ajili ya kutafuta haki,” alisema Hakimu Odira.

Akihojiwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Tumaini Kweka, shahidi huyo wa utetezi alidai mahakamani huko, kwamba hakuwahi kuandika maelezo yoyote kituo cha polisi wala kuhojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupata na Rushwa (TAKUKURU).

Katika hatua nyingine Wakili Kweka, aliiomba mahakama hiyo, kutumia kifungu namba 154 cha sheria ya ushahidi kutumia maelekezo ya shahidi aliyoandika kituo cha polisi kumhoji.

Wakili huyo wa Serikali, aliieleza mahakama kwamba kwa mujibu wa utaratibu wa kisheria maelezo hayo yanaweza kuwa ya shahidi au kumhusu mwenyewe, pia siyo lazima maelezo yawe yameandikwa na shahidi na wakati mwingine siyo lazima aonyeshwe maelezo hayo mahakamani kwa kuwa ni takwa la kisheria.

Chanzo: Nipashe