Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya Padri anayedaiwa kubaka kuanza wiki ijayo

Padre Mtuhumiwa ubakaji adri Erasmus Swai.

Thu, 12 Aug 2021 Chanzo: ippmedia.com

MAHAKAMA ya Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, imepanga Agosti 17, mwaka huu, kuanza kusikiliza shauri la ubakaji na kumsababisha ujauzito mwanafunzi wa kidato cha nne, linalomkabili aliyekuwa Paroko wa Parokia ya Manushi ya Kanisa Katoliki, Jimbo la Moshi, Padri Erasmus Swai.

Taarifa ya kuanza kwa kesi hiyo, iliwekwa wazi jana na Hakimu Mkazi, Thurston Kombe wa wilaya hiyo, baada ya mahakama kumhoji mshtakiwa kama yuko tayari kusomewa maelezo ya awali.

Kesi hiyo namba sita ya mwaka huu, awali ilikuwa ikipigwa kalenda mara kwa mara kutokana na upelelezi wake kutokamilika na jalada lake kupelekwa katika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS) kwa ajili ya mapitio.

Baada ya Hakimu Kombe kumhoji mshtakiwa kutokana na wakili wake kutokuwapo mahakamani, aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 17, mwaka huu.

Kesi hiyo inayovuta hisia za waumini wengi wa utawala wa sheria na wapenda haki, mshtakiwa (Padri Swai), anatetewa na Wakili Monica Denisi.

Padri Swai, anadaiwa kutenda makosa hayo kwa mtoto mwenye umri wa miaka 17, ambaye ni Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kimaseki iliyopo mkoani Arusha.

Katika hati ya mashtaka, inadaiwa kuwa Machi mwaka jana akiwa katika Hoteli ya Snow View iliyopo katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Hai, kwa nyakati tofauti, Padri Swai alimbaka mwanafunzi huyo.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, mshtakiwa alitenda kosa la kwanza la kubaka chini ya

Wakati kosa la pili ni kumpa ujauzito mwanafunzi huyo, kinyume na kifungu cha 60 (A) (3), Sura ya 353 cha Sheria ya Elimu.

Chanzo: ippmedia.com