Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya Muharami yaahirishwa hadi Februari 15

Hukumu Pc Data Kesi ya Muharami yaahirishwa hadi Februari 15

Thu, 2 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Upande wa mashtaka katika kesi inayomkabili mfanyabiashara, Muharami Abdullah maarufu kama Chonji umedai kuwa wapo kwenye maandalizi ya kuandaa maelezo ya mashahidi na vielelezo.

Chonji na wenzake wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin na cocaine zenye thamani ya Sh328 milioni.

Wakili wa Serikali, Caroline Matemu alidai mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa shauri lilikuja kwa ajili ya kutajwa, hivyo wapo kwenye maandalizi ya kuandaa mashahidi na vielelezo ili waweze kuwasomea

“Bado tupo kwenye maandalizi ya kuandaa maelezo ya mashahidi na vielelezo, hivyo tunaomba mahakama hii ihairishe shauri hili,” alidai Matemu.

Hakimu mwandamizi, Rhoda Ndimilanga aliahirisha shauri hilo hadi Februari 15 kwa ajili ya kutajwa.

Washtakiwa wengine katika shtaka hilo ni Abdul Chumbi, Rehani Umande, Tanaka Mwakasagule na Maliki Maunda wote wakazi wa Magomeni Makanya.

Washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa Oktoba 21, 2014 katika eneo la Magomeni Makanya Wilaya ya Kinondoni, walisafirisha dawa za kulevya aina ya heroin zenye uzito wa gramu 5,309.57, zikiwa na thamani ya Sh265, 478,500.

Shtaka la pili, siku na eneo hilo, washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya cocaine zenye uzito wa gramu 894.28, zikiwa na thamani ya Sh 62,599,600.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live