Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya Mbowe yapamba moto, Mawakili wawasilisha mapingamizi matatu

MBOWE12 Freeman Aikael Mbowe, Mwenyeketi wa CHADEMA

Wed, 1 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake wawili, iliyopo katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, maaarufu kama Mahakama ya Mafisadi, imeahirishwa hadi Septemba 3, 2021, kwa ajili ya upande wa mashtaka kuja kujibu pingamizi lililowasilishwa na washtakiwa.

Ni baada ya wakili wa utetezi, Peter Kibatala kuwasilisha mahakamani hapo mapingamizi matatu likiwemo la hati hiyo kuwa ina makosa.

Pingamizi jingine ni makosa mawili ya kula njama yaliyopo katika hati ya mashtaka ya wateja wake, yametenganishwa badala ya kuwa kosa moja.

Pia mahakama hiyo inakosa mamlaka ya kuendesha mashtaka yanayowakabili washtakiwa wote kwa sababu kifungu cha 4 cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi ya Mwaka 2002, ambacho ndiyo kina weka zuio zaidi ya makosa ya ugaidi nchini Tanzania, hakifafanui ni vitu gani au viashiria gani vinavyotengeneza ugaidi.

Kibatala baada ya kuwasilisha mapingamizi hayo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando aliiomba mahakama iwape muda wa kupitia mapingamizi hayo na kisha kuja kujibu hoja hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live