Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya Mbowe kutumia mashahidi 24

MBOWE MBOWE Freeman Aikael Mbowe, Mwenyeketi wa CHADEMA

Mon, 23 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashahidi 24 na vielelezo 19 wanatarajia kutoa ushahidi katika kesi ya Ugaidi inayomkabili, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu

Miongoni mwa mashahidi hao, yupo aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai nchini (DCI), Robert Boaz

Hayo yameelezwa leo, Agosti 23, 2021 na upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga akisaidiana na Ester Martin, wakati wakiwasomea maelezo ya mashaidi na vielelezo( Commital Proceedings) washtakiwa hao, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba

Chanzo: www.tanzaniaweb.live