Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya Mbowe: Afande Msemwa amaliza kutoa ushahidi

Mbowe.png?fit=680%2C510&ssl=1 Kesi ya Mbowe: Afande Msemwa amaliza kutoa ushahidi

Mon, 20 Sep 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

LEO Jumatatu, Septemba 20, 2021 Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Dar es Salaam imeahirisha kesi ya Ugaidi na Uhujumu Uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu Septemba 24, 2021.

Shahidi wa pili katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi, inayomkabili Mbowe na wenzake watatu alikuwa Mkaguzi wa Jeshi la Polisi Mahita Mahita, ambaye amemaliza kutoa ushahidi wake leo mbele ya Jaji Mustapha Siyani.

Shauri hilo dogo lilitokana na mapinganizi ya mawakili wa utetezi, wakiongozwa na Wakili Peter Kibatala, wakipinga maelezo ya onyo ya mshtakiwa wa pili katika kesi ya msingi, Adam Kasekwa, yasitumike mahakamani hapo kama kielelezo na Kamanda Kingai, katika kesi ya msingi, wakidai yalichukuliwa nje ya muda kisheria.

Pia, katika mapingamizi hayo walihoji kwa nini mtuhumiwa alihojiwa Dar es Salaam, badala ya Moshi mkoani Kilimanjaro alikokamatwa. Mbowe na mwenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka sita yakiwemo ya kula njama na kufadhili fedha kwa ajili ya vitendo vya kigaidi.

Baada ya hapo, shahidi wa tatu katika kesi hiyo ambaye ni askari polisi mwenye namba H 4323 Constable Msemwa kutoka Kituo Cha Polisi Oysterbay, alianza kutoa ushahidi wake akiongozwa na wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga, mbele ye Jaji Mustapha Siyani anayesikiliza shauri hilo.

Baada ya Msemwa kumaliza kutoa ushahidi wake, shahidi wa nne wa upande wa Serikali aliyetarajiwa kufika mahakamani hapo kuendelea kutoa ushahidi ameshindwa kutoakana na kupata dharura ya kiafya hivyo kesi imeahirishwa hadi Septemba 24, 2021.

Mbowe na mwenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka sita yakiwemo ya kula njama na kufadhili fedha kwa ajili ya vitendo vya kigaidi.

Chanzo: globalpublishers.co.tz