Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya Makonda, Lemutuz kutajwa Disemba 8

Makonda Lemutuz.jpeg Kesi ya Makonda, Lemutuz kutajwa Disemba 8

Wed, 23 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kesi ya tuhuma za uporaji wa gari aina ya Range Rover, inayomkabili aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paulo Makonda na mmiliki wa blogu ya Lemutuz, William Malecela imepangwa kutajwa Desemba 8, 2022.

 Ni baada ya Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate kuwa kwenye majukumu mengine ya kikazi.

Shauri hilo limefunguliwa na mfanyabiashara, Patric Kamwelwe akidai alipwe fidia ya zaidi ya Sh 240 miliini ambazo ni gharama za kodi thamani ya gari hilo la kifahali.

Wakili Wabeya Kung'e anayemwakilisha Kamwelwe alidai mbele ya hakimu alidai shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kutajwa.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Mkazi Mkuu, Mery Mrio amesema hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate anayesikiliza shauri hilo yupo kwenye majukumu mengine ya kikazi hivyo ameahirisha shauri hilo hadi Disemba 8,2022 kwa ajili ya kutajwa.

Kwa upande wa Makonda, akiwakilishwa na Wakili Simon Mbawala huku Limutuz akiwakilishwa na wakili Ruben Simwanza.

Katika hati ya madai ya mfanyabishara huyo anadai yeye na Lemutuz ni marafiki alitumia urafiki wake kumkabidhi Makonda gari aina ya Range Rover

Mfanyabiashara huyo alimkabidhi gari hilo Lemutuz ili ampatie Makonda aweze kutumia wakati akiwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa makubaliano alitumie kwa wiki mbili na kisha amrudishie.

Lakini imekuwa tofauti na makubaliano hayo ambapo Makonda ameendelea kulitumia gari hilo mpaka Leo hii hajamrudishia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live