Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya 'Maafisa Usalama' Feki kuanza Mei 5

RUNGU Watuhumiwa wako nje kwa dhamana

Thu, 21 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakaka ya Hakimu Mkazi Kisutu, imepanga Mei 5, 2022 kuanza kusikiliza ushahidi katika kesi ya kujifanya maofisa Usalama wa Taifa (TISS) inayomkabili mfanyabiashara Joshua Kamalamo (37) na mwenzake Yahaya Kapalatu (31).

Kamalamo na Kapalatu wanadaiwa kujitambulisha kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini Tanzania (DPP), Sylvester Mwakitalu na Naibu wake, Joseph Pande kuwa ni wao ni maofisa wa usalama wa Taifa( TISS) wakati wakijua kuwa ni uongo.

Uamuzi huo umetolewa leo Alhamisi April 21, 2022 na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Rhoda Ngimilanga, wakati shauri hilo lilipoitwa mahakamani hapo kwa ajili ya kuanza kusikilizwa ushahidi.

Kabla ya kupangwa kwa tarehe hiyo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Grace Mwanga amedia kuwa shauri hilo limepelekwa mahakamani hapo kwa ajili ya kuanza kusikiliza, lakini hakimu anayesikikiza shauri hilo, Godfrey Isaya, ana udhuru.

" Kutokana na sababu hiyo, tunaomba Mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kuanza ushahidi" ameeleza Wakili Mwanga.

Wakili Mwanga baada ya kueleza hayo, Hakimu Ngimbilanga ameahirisha kesi hiyo hadi Mei 5, 2022 itakapoanza kusikilizwa. Washtakiwa wapo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana ambayo kila mshtakiwa alipaswa kuwa na wadhamini wawili wenye barua kutoka taasisi inayotambuliwa kisheria watakao saini bondi ya Sh 7milioni.

Katika kesi ya msingi, washitakiwa wanakabiliwa na kesi ya jinai namba 99/2021, ambapo wanadaiwa kutenda makosa hayo Juni 12, 2021 katika ofisi za DPP zilizopo katika jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani, Jijini Dar es Salaam.

Inadaiwa siku hiyo ya tukio, washitakiwa hao wakiwa katika ofisi hiyo, walijitambulisha kwa (DPP) Slyvester Mwakitalu na Naibu wake, Joseph Pande kwamba wao ni maofisa wa usalama wa Taifa (TISS), wakati wakijua kuwa ni uongo.

Kwa mara ya kwanza, washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo, Juni 2021 na kusomewa mashtaka mawili ya kujitambulisha kuwa wao ni maofisa usalama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live