Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya Jamii Forum yashindwa kuendelea

46674 Jamii+pic

Thu, 14 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Kesi ya kuzuia jeshi la polisi kufanya uchunguzi, inayomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jamii Forum, Maxence Melo na mwenzake Micke William, imeshindwa kuendelea na utetezi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Patrick Mwita ameeleza leo Alhamisi Machi 14, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba, kuwa shauri hilo limekuja kwa ajili ya kusikilizwa.

Wakili wa utetezi, Jeremiah Mtobesya amedai kuwa upande wa utetezi ulishindwa kuandaa mashahidi jana kutokana na kuwa na kesi nyingine Mahakama Kuu.

"Shauri limekuja kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa lakini mimi na wakili mwenzangu (Peter) Kibatala tulishindwa kuandaa mashahidi jana kutokana na kuwa na kesi Mahakama Kuu, hivyo tunaomba tarehe nyingine," amedai Wakili Mtobesya.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba ameahirisha shauri hilo hadi Machi 19, 2019 na kuutaka upande wa utetezi kuleta mashahidi ili kesi hiyo ikamilike kwa kuwa ni ya muda mrefu toka ilipofunguliwa Desemba 19, 2016.

Tayari mashahidi wanne wa upande wa mashtaka wameshatoa ushahidi wao dhidi ya washtakiwa hao na Mahakama kuwakuta na kesi ya kujibu.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa wanadaiwa kuzuia jeshi la Polisi kufanya uchunguzi, kinyume na Sheria Namba 22 (2) cha Sheria ya Makosa ya Mtandano Namba 14 ya mwaka 2015.

Washtakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo, kati ya Aprili Mosi, 2016 na Desemba 13, 2016 katika maeneo ya Mikocheni wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.

 Soma zaidi>> Kesi ya Jamii Forum yakwama tena mahakamani

   >>Kigogo Jamii Forum, mwenzake wana kesi ya kujibu



Chanzo: mwananchi.co.tz