Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya Halima Mdee yakwama mahakamani

Wed, 12 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Kesi ya kutoa lugha chafu dhidi ya Rais wa Tanzania John Magufuli inayomkabili Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee imeshindwa kuendelea katika Mahakama  ya Hakimu Mkazi Kisutu kutokana na kuwa mgonjwa.

Wakili wa Serikali, Silvia Mitanto amedai leo Jumanne Juni 11,2019 mbele ya  Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kusikilizwa lakini mshtakiwa ni mgonjwa na mdhamini wake yupo.

Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 9 mwaka 2019 kwa ajili ya kuendelea na usikilizaji.

Mpaka sasa mashahidi watatu wa upande wa mashitaka wameshatoa ushahidi katika kesi hiyo akiwamo Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Urafiki, Mrakibu wa Polisi (SP) Batseba Kasanga.

Katika kesi ya msingi inadaiwa Julai 3, 2017 katika ofisi za makao makuu ya Chadema zilizopo mtaa wa Ufipa wilayani Kinondoni, Mdee alitamka maneno dhidi ya  Rais John Magufuli kuwa,  ‘anaongea hovyo, anatakiwa  afungwe breki,’ kitendo kinachodaiwa kuwa ni kumdhalilisha Rais na kusababisha uvunjifu wa amani.

 

Pia Soma



Chanzo: mwananchi.co.tz