Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya Gugai yapigwa kalenda

27087 Pic+gugai TanzaniaWeb

Wed, 14 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kuendelea kuisikiliza kesi ya utakatishaji fedha na kumiliki mali zilizozidi kipato inayomkabili aliyekuwa  Mhasibu Mkuu wa Takukuru, Godfrey Gugai na mwenzake, baada ya mashahidi wa upande wa mashtaka kuwa na dharura.

Wakili wa serikali Mkuu, Vitalis Peter Leo Novemba 14, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amedai kuwa kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kuendelea kusikiliza kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka lakini hawapo tayari.

Kwa sababu wamepata taarifa kuwa shahidi waliyemtarajia kutoa ushahidi katika kesi hiyo amepatwa na dharura na kwamba tatizo linalomkabili halijatatulika na hivyo wakili Peter aliiomba Mahakama waandae ushahidi mwingine ili waweze kuendelea naye.

Baada ya Wakili Peter kueleza hayo, Hakimu Simba alisema, “kwa mtindo huu hii kesi haitomalizika sasa hivi, tutakuwa tunacheza tu.

Hakimu Simba aliongeza, “sasa muwe mnaleta mashahidi wawili wawili ili mmoja akipata dharura mwingine anaendelea na kwamba hali kama hiyo imekwisha jitokeza zaidi ya mara nne ama tano.

Upande wa utetezi ukiwakilishwa na mawakili Alex Mgongolwa, Semi Malimi, Nduluma Majembe, Denis Tumain na John Mhozya.

Kwa upande wake wakili Mgongolwa alitaka mashahidi wanaokwenda kutoa ushahidi katika kesi hiyo wajulikane na kwamba upande wa mashtaka unapoona shahidi wanayemtafuta ana tatizo watafute mwingine.

Hakimu Simba alisisitiza upande wa mashtaka kupelekwa mahakamani hapo mashahidi wawili wawili na kuiahirisha kesi hadi Novemba 27 na 28, mwaka huu ambapo wataendelea kusikiliza kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka. Mbali na Gugai, washtakiwa wengine katika hiyo ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasin Katera.

Katika kesi hiyo, Gugai na wenzake, wanakabiliwa na makosa 43, kati ya hayo 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali.

Tayari shahidi  wawili wa upande wa mashtaka, wameshatoa ushahidi wao miongoni mwa mashahidi hao ni Ayoub Akida (52) ambaye ni Ofisa Utumishi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Boniface Sechuma kutoka Takukuru Makao Makuu Dodoma. 

Miongoni mwa mashtaka yanayomkabili Gugai ni kosa la kumiliki mali zilizozidi kipato chake halali, ambapo anadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Januari 2005 na Desembea 2015.



Chanzo: mwananchi.co.tz