Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya Dk Pima, wenzake yapigwa kalenda

PIMA Kesi ya Dk Pima, wenzake yapigwa kalenda

Thu, 11 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, imepiga kalenda kesi za uhujumu uchumi zinazomkabili aliyekuwa mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Dk John Pima na wenzake wanne hadi Agosti 18, 2022.

Leo Alhamisi Agosti 11, 2022, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Janeth Sekule ameieleza Mahakama hiyo ilipanga kuanza kusikiliza kesi mbili kati ya tatu zinazowakabili kwa kuwasomea maelezo ya awali.

Mbali na Dk Pima, washitakiwa wengine ni aliyekuwa mkuu wa idara ya mipango na uchumi, Innocent Maduhu, aliyekuwa Mkuu wa idara ya fedha katika halmashauri hiyo, Mariam Mshana, Nuru Ginana (aliyekuwa mchumi) na Alex Daniel.

Mbele ya Hakimu Mkazi, Regina Oyier, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Janeth Sekule, ameieleza mahakama katika kesi ya uhujumu uchumi namba 3/2022 inayomkabili Dk Pima, Mshana, Maduhu na Ginana ilipangwa kwa ajili ya kuwasomea watuhumiwa hao maelezo ya awali.

Wakili huyo aliomba mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kuwasomea washitakiwa hao maelezo hayo mbele ya Hakimu anayesikiliza kesi hiyo.

Hakimu Oyier alieleza kuwa Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Fadhil Mbelwa, anayesikiliza shauri hilo ana majukumu mengine hivyo kuahirisha hiyo.

Aidha kesi nyingine ya uhujumu uchumi namba 4/2022 inayomkabili Dk Pima,Mshana,Maduhu na Daniel,ambayo pia ilipangwa kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali,inayosikilizwa na Hakimu Mbelwa iliahirishwa ambapo ilipangwa kwa ajili ya kuwasomea washitakiwa hao maelezo ya awali.

Watuhumiwa hao katika kesi hizo mbili watuhumiwa hao wanakabiliwa na makosa nane ikiwemo ya ufujaji na ubadhirifu pamoja na makosa la matumizi ya nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajiri.

Katika kesi ya uhujumu uchumi namba 5/2022, inayomkabili Dk Pima,Mshana na Maduhu,Wakili Sekule aliiambia mahakama kuwa upelelezi wa shauri bado haujakamilika hivyo anaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Kwenye kesi hiyo watuhumiwa hao wanakabiliwa na makosa sita ikiwemo kosa la utakatishaji fedha Sh103 milioni ambapo wanadaiwa kujipatia fedha hizo huku wakijua ni zao la uhalifu la kosa la kutumia nyaraka kumdanganya mwajiri wao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live