Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya Chonji na wenzake, Serikali bado inaandika maelezo ya shahidi

Hukumu Pc Data Kesi ya Chonji na wenzake, Serikali bado inaandika maelezo ya shahidi

Mon, 19 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesema wanamalizia kuandika maelezo ya shahidi mmoja ndio waandae taarifa muhimu katika kesi ya kusafirisha dawa kulevya inayomkabili mfanyabiasha maarufu nchini, Muharami Abdallah maarufu kama Chonji na wenzake wanne.

Taarifa hiyo muhimu baada ya kuiandaa, wataiwasilisha Mahakama Kuu ili iweze kupitiwa na kutolewa maamuzi kabla ya washtakiwa kusomewa maelezo ya mashahidi na vilelelezo (Commital Proceedings).

Chonji na wenzake wakabiliwa na mshataka mawili ya kusafirisha dawa za kulevya aina Heroin na Cocaine zenye thamani ya Sh328 milioni.

Wakili wa Serikali, Erick Kamala ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Jumatatu Juni 19, 2023 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Mary Mrio wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.

"Mheshimiwa hakimu tarehe iliyopita, washtakiwa walisema wanataka kujua kesi yao imefikia hatua gani? Sasa kwa ufupi nimeambiwa wanamalizia kuandika maelezo ya shahidi mmoja halafu ndio waandae taarifa muhimu kwa ajili ya kuwasilisha Mahakama Kuu," amedai Kalama.

Wakili Kamala baada ya kueleza hayo, ameomba mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Mrio baada ya kusikiliza maelezo hayo, ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 3, 2023.

Hata hivyo kesi hiyo imeahirishwa kwa njia ya video.

Mbali na Abdallah washtakiwa wengine katika shauri hilo ni Abdul Chumbi, Rehani Umande, Tanaka Mwakasagule na Maliki Maunda wote wakazi wa Magomeni Makanya.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa Oktoba 21, 2014 katika eneo la Magomeni Makanya wilaya ya Kinondoni, walisafirisha dawa za kulevya aina ya heroin zenye uzito wa gramu 5309.57, zikiwa na thamani ya Sh265, 478,500.

Shtaka la pili, siku na eneo hilo, washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kusafirisha dawa za kulevya aina Cocaine zenye uzito wa gramu 894.28, zikiwa na thamani ya Sh62,599,600.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live