Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya Bilionea Msuya kuendelea kusikilizwa leo

Kesi Ya Bilionea Msuya Kuendelea Kusikilizwa Leo Kesi ya Bilionea Msuya kuendelea kusikilizwa leo

Tue, 15 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kesi ya mauaji ya mdogo wa marehemu, Erasto Msuya maarufu kwa jina la Bilionea Msuya, Aneth Msuya inatarajia kuendelea kusikilizwa leo kwa upande wa mashahidi wa Jamhuri katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Washitakiwa katika kesi hiyo namba 103 ya mwaka 2018 ni mke wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu wa madini mkoani Arusha, marehemu Erasto Msuya, Miriam Mrita na mfanyabiashara Revocatus Muyela wote wakazi wa mkoani Arusha.

Kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa jana mbele ya Jaji Edwin Kakolaki wa mahakama hiyo, lakini ilishindikana kwa sababu Wazee wa Baraza katika kesi hiyo hawakuwepo, walikuwa kwenye kesi nyingine wanasikiliza.

Kutokana na hali hiyo, kesi hiyo iliahirishwa hadi leo kwa ajili ya kusikilizwa.

Washitakiwa wanawakilishwa na Wakili Peter Kibatala na Nehemiah Nkoko na kwa upande wa mashitaka unawakilishwa na Yasinta Peter.

June 27, 2023 kesi hiyo iliahirishwa hadi kikao kingine cha mahakama kitakachopangwa na msajili, kwa sababu upande wa mashitaka haukuwa na mashahidi watatu mfulululizo, ambapo hadi washitakiwa kupangiwa kiko hicho walikaa miezi 15 ndiyo wakapangiwa.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Yasinta Peter kuomba ahirisho kwa sababu hawana shahidi kwa siku zote zilizobaki, shahidi waliyomtegemea atoe ushahidi wake ili na wengine wafuatie bado ni mgonjwa.

Alidai kuwa walifahamishwa kuwa, Dk Felidelis Segumba bado ni mgonjwa na anaruhusa ya matibabu nchini India kuanzia Mei 29 hadi Juni 20,2023, baada ya kurudi amepata mapumziko ya kiafya na ataweza kufika kutoa ushahidi wake Julai 10,2023.

Baada ya Peter kudai hayo, Wakili wa mshitakiwa wa kwanza Miriam, Peter Kibatala alidai kuwa kwa mazingira hayo hawana pingamizi na ahirisho, pia kwa upande wa Muyela, wakili wake, Nehemiah Nkoko naye alidai hana pingamizi.

" Kutokana na sababu zilizotolewa na upande wa Jamhuri na ukweli kwamba kikao hiki kilipangwa kumalizika Juni 30,2023 kwa maana ya Ijumaa ni wazi kwamba hatutaweza kuendelea na kusikilizwaji,"

"Kwa hiyo na ahirisha shauri hili hadi kikao kingine kijacho cha mahakama kitakachopangwa na msajili, ambapo pande zote zitajulishwa”alisema Jaji Kakolaki

Chanzo: www.tanzaniaweb.live