Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya Aveva, Godfrey Nyange Kaburu zapigwa kalenda

5828 Rais Wa Simba.png TZW

Thu, 5 Apr 2018 Chanzo: bongo5.com

Kesi inayowakabili viongozi wa klabu ya Simba SC, Evans Aveva na Godfrey Nyange Kaburu imehairishwa mpaka  Aprili 12  mwaka 2018.

Rais wa Simba SC, Aveva ambaye anasumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu amefika katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuhudhuria kesi yake inayomkabili ambapo jana alipaswa kusomewa maelezo ya awali na mwenzake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.
Licha ya kusomewa maelezo hayo, kesi hiyo imeahirishwa tena mpaka Aprili 12  mwaka 2018 kufuatia Wakili wa TAKUKURU, Leonard Swai, kuomba hati ya mashtaka ifanyiwe mabadiliko.
Swai ameiomba Mahakama kubadilisha hati ya mashtaka kwa kumuongeza mshtakiwa mwingine ambapo Aprili 12 mwaka 2018 watasomewa maelezo hayo ya awali.
Taarifa zinaeleza kuwa hatua hiyo imefikia hapo baada ya upelelezi kukamilika upande wa mashtaka.
Mhusika mwingine anayekabiliwa na kesi hiyo ni Makamu wa Rais wa Simba, Godfrey Nyange Kaburu ambaye alitinga pia mahakamani hapo leo.
Washtakiwa wote wawili wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi nyaraka za uongo na utakatishaji wa fedha, kiasi cha USD 300,000.
Chanzo: bongo5.com