Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi wanaodaiwa kuwa wafuasi Chadema yakwama

Sun, 19 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Ijumaa Mei 17, 2019 imeshindwa kuwasomea maelezo ya awali washtakiwa 16 wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Chadema kutokana na washtakiwa watatu kutofika mahakamani na kutoa udhuru.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na shtaka moja la kufanya mkusanyiko usio halali.

Awali washtakiwa hao walikuwa 31 lakini 15 waliruka dhamana ambapo Mahakama ilishatoa hati ya kukamatwa.

Wakili wa Serikali Faraji Nguka amedai leo Mei 17, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi, Agustin Ruizile kuwa kesi jiyo imekuja kwa ajili ya uamuzi wa mahakama baada ya kuomba shauri hilo kuendelea bila washtakiwa 15 kutokuwepo.

Wakili wa utetezi,  Alex Massaba amedai kuwa  tayari kuwawakilisha washtakiwa 16 waliopo mahakamani na kujitoa kuwawakilisha washtakiwa 15 ambao wameruka dhamana.

Wakili Nguka alieleza kwa mujibu wa sheria ya makosa ya jinai kifungu cha 192(1) kinaeleza kuwa mtuhumiwa anaposomewa hoja za awali anatakiwa kuwepo mwenyewe mahakamani na sio kuwakilishwa.

Pia Soma

"Kuna baadhi ya washtakiwa wadhamini wao wamefika kutokana  na sheria inavyosema tunaomba kesi hii iahirishwe ili washtakiwa wote waweze kuwepo wakati wa kusomewa hoja za awali,” amedai wakili Nguka.

Massaba alikubaliana na hoja za upande wa mashtaka na kuomba kesi hiyo kupangiwa tarehe nyingine ili washtakiwa wote wawepo.

Hakimu Rwizile ameahirisha kesi hiyo hadi Juni 4, 2019 na kuwataka washtakiwa wote kuwepo kwa ajili ya kuwasomea hoja za awali.

Washtakiwa katika kesi hiyo ya jinai namba 51 ya  mwaka 2018,  ni Thabita Mkude, Haji Lukwambe, Emmanuel Kimoi,Mohammed Juma, Hussein Mrombo, Abdallah Hamis, Hussein Kidda, Paulo Kimoro, Brayan Morris, Hussein Nguli na Edna Kimoro.

Wengine ni  Jonathan Lema, Salha Ngondo, Ramadhan Mombo, Godwin Mwakasungura, Hassan Kibweda, Omary Hamad, Fatima Ramadhan, Ezekiel Nyenyembe, Denis Mtegwa, Dickson Kerefu, Raphael Mwaipopo, Athuman Mkawa, Mussa Kusigila.

Wengine ni Omary Danga, Jackson Masilingi, Asha Kileta, Ally Rajabu,  Isack Ng'aga, Erick John na Aida Olomi.

Kwa pamoja wanadaiwa kuwa Februari16, 2018 Kinondoni katika eneo la Mkwajuni Wilaya ya Kinondoni walifanya mkusanyiko usio wa halali na kinyume cha sheria.

Ilidaiwa kuwa mkusanyiko huo ulikuwa na nia yakufanya uvunjifu wa amani na kusababisha taharuki kwa wananchi.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz