Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi wanaodaiwa kusafirisha kilo 268 heroin yaiva

Hukumu Pc Data Kesi wanaodaiwa kusafirisha kilo 268 heroin yaiva

Tue, 9 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Upelelezi wa kesi ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin zenye uzito wa kilo 268.50 inayowakabili watu watatu akiwemo raia wa Nigeria, David Chukwu, umekamilika.

Wakili wa Serikali, Erick Davies ametoa maelezo hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Aaron Lyamuya wa Hakimu Mahakama ya Mkazi Kisutu, leo Januari 8, 2024 wakati kesi ya uhujumu uchumi namba 36/2020 ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.

Kutokana hali hiyo wakili Davies ameomba mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kuwasilisha taarifa Mahakama Kuu.

Hakimu Lyamuya aliahirisha hadi kesho, kwa ajili ya kutajwa.

Mbali na Chukwu, ambaye ni mkazi wa Masaki, washtakiwa wengine ni Isso Lupembe(49) mfanyabiashara na mkazi wa Mbezi Luis pamoja na Allistair Mbele(38), mkazi wa Mbezi Kibanda cha Mkaa.

Washtakiwa kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili, ambayo ni kusafirisha dawa za kulevya na kutakatisha fedha kiasi cha Sh17.8 milioni.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa wanadaiwa Aprili 15, 2020 eneo la Kibanda cha Mkaa lililopo wilaya ya Ubungo, kwa pamoja wanadaiwa kukutwa wakisafirisha dawa za kulevya aina ya heroin zenye uzito wa kilo 268.5 wakati wakijua ni kosa kisheria.

Shitaka la pili ni kutakatisha fedha, tukio wanalodaiwa kulitenda kati ya Januari Mosi, 2016 na April 15, 2020 katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.

Inadaiwa katika kipindi hicho, washtakiwa walijihusisha na miamala tofauti tofauti ya fedha ambayo ni zaidi ya Sh17.83 milioni, huku wakijua fedha hizo ni zao tangulizi la kosa la kusafirisha dawa za kulevya.

Kwa mara ya kwanza, washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo April 24, 2020 na kusomewa mashtaka yao.

Kutokana na mashtaka yanayowakabili washtakiwa hao hawana dhamana kwa mujibu wa sheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live