Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi uvamizi wa Kanisa yaendelea kupigwa kalenda

Kanisa Geita Kesi Kesi uvamizi wa Kanisa yaendelea kupigwa kalenda

Thu, 25 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kesi inayomkabili Elpidius Edward (22) mkazi wa Mtaa wa Katundu mjini Geita anaedaiwa kuvamia Kanisa Kuu la Kiaskofu Jimbo la Geita na kufanya uharibifu wa mali zenye thamani ya Sh48.2 milioni imeendelea kupigwa kalenda.

Kesi hiyo imeendelea kusogezwa mbele baada ya Mwanasheria wa Serikali anayeisimamia kuwa kwenye vikao vya Mahakama kuu Mwanza.

Hii ni mara ya pili kesi hiyo kushindwa kusikilizwa baada ya Mei 10, 2023, Wakili huyo kushindwa kuhudhuria mahakmani kwa madai ya kuwa kwenye vikao vya Mahakama Kuu vinavyoendelea mkoani Mwanza.

Kesi hiyo namba 62/2023 imekuja katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita kwa ajili ya shahidi wa pili kuendelea kutoa ushahidi wake.

Akitoa ombi la ahirisho la kesi hiyo Wakili wa Serikali, Musa Mlawa ameieleza Mahakama kuwa hawatakuwa na shahidi kutokana na wakili anaeisimamia kuwa na vikao vya kesi Mahakama Kuu na kuomba kupangiwa tarehe nyingine.

Kufuatia ombi hilo Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Johari Kijuwile ameiahirisha hadi Juni 7, 2023 itakapokuja kwa ajili ya upande wa mashtaka kuita mashahidi wengine.

Mshatakiwa Elpidius, Mkazi wa Geita anashtakiwa kwa makosa mawili ikiwemo la kuingia katika jengo la Kanisa Katoliki Geita kinyume na kifungu cha 294 (1) na (2) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2022.

Katika shtaka la pili mshtakiwa huyo anadaiwa kuharibu mali zenye thamani ya Sh 48.2 milioni kinyume na kifungu namba 226 (1) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2022.

Mshatakiwa amerudishwa mahabusu kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya dhamana yaliyomtaka kuwa na wadhamini wawili watakaosaini hati ya fedha taslimu Sh24.1 milioni au mali isiyo hamishika yenye thamani hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live