Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi mke wa Bilionea Msuya hadi Julai 23

11176 KESI+PIC.png TanzaniaWeb

Tue, 10 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Upande wa mashtaka katika kesi ya mauaji inayomkabili Miriam Mrita (41), mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa jalada la kesi bado lipo mikononi kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Wakili wa Serikali mwandamizi, Patrick Mwita alieleza hayo jana mbele ya Hakimu Thomas Simba shauri lilipotajwa jana.

Mbali na Miriam (pichani) shtakiwa mwingine katika kesi hiyo ya mwaka 2017, ni mfanyabiashara Revocatus Muyela (40). Wanadaiwa kumuua Aneth Msuya ambaye ni dada wa Erasto Msuya.

Baada ya Mwita kueleza hayo, wakili wa utetezi Omari Msemo alikubali ombi hilo na kuishauri mahakama kupanga tarehe za karibuni. Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 23, itakapotajwa.

Washtakiwa wanadaiwa kutenda mauaji hayo Mei 25, 2016 maeneo ya Kibada Kigamboni, Dar es Salaam.

Chanzo: mwananchi.co.tz