Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi meno 413 ya tembo yapigwa kalenda

Meno Ya Tembo Kesi meno 413 ya tembo yapigwa kalenda

Tue, 15 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kesi ya kununua, kuuza, kumiliki na kusafirisha meno 413 ya tembo na vipande 2 vya meno ya kiboko inayowakabili washtakiwa saba imeshindwa kuendelea baada ya shahidi aliyetegemewa kutoa ushahidi kudaiwa kuwa hospitalini.

Wakili wa Serikali Monica Ndakidemu ameeleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Evodia Kyaruzi

Wakili huyo amedai kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kusikiliza ushahidi lakini shahidi aliyekuwa akitegemewa kutoa ushahidi yupo hospitali.

"Tunaiomba mahakama hii ipange tarehe nyingine ya usikilizwaji Kwa kuwa leo hii hatuna shahidi na tuliyemtegemea yupo hospitali,"amedai Ndakidemu.

Washitakiwa katika kesi hiyo ni Hamis Abdallah, Hassan Likwena(39), Bushiri Likwena, Oliver Mchuwa (35), Haidary Sharifu(44), Joyce Thomas(33) na Salama Mshamu(21) wote ni wakazi wa Dar es Salaam.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 29, 2023 huku watuhumiwa wakiwa mahabusu Kwasababu mashtaka yanayowakabili ni ya uhujumu uchumi.

Katika kesi ya msingi inadaiwa kuwa Januari Mosi, 2017 na Septemba 2, 2019 washtakiwa wote kwa pamoja katika Mikoa wa Mtwara ,Pwani na Dar es Salaam waliongoza genge la uhalifu, walipanga kuuza, Kununua, kumiliki na kusafirisha meno 413 ya tembo pamoja na vipande viwili vya meno ya kiboko vyenye thamani ya zaidi ya Shi4.3 bilioni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live