Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi mauaji ya Alphonce Mawazo wa Chadema yahamia Mahakama Kuu

73333 Mawazopic

Wed, 28 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Geita. Washtakiwa watano wa kesi ya mauaji ya aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema mkoani Geita, Alphonce Mawazo wamefikishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza leo Jumatano Agosti 28, 2019.

Leo ni mara ya kwanza kwa kesi hiyo kusikilizwa mahakama kuu baada ya kuhamishwa kutoka mahakama ya hakimu mkazi Geita ambayo haina sifa ya kusikiliza kesi ya mauaji.

Katika kesi hiyo namba 8 ya mwaka 2019  iliyosikilizwa katika mahakama ya hakimu mkazi Geita, kwa pamoja wanashtakiwa kwa kosa la mauaji kifungu namba 196 ya sheria ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Kesi hiyo inasikilizwa na Omary Kingwele, naibu msajili  wa mahakama kuu aliyepewa mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.

Polisi: Marufuku kukusanyika kuaga mwili wa Mawazo

Akisoma maelezo ya awali wakili wa Serikali mwandamizi, Hemed Halidi akishirikiana na Clemency Katto ameieleza mahakama hiyo kuwa Novemba 14, 2015 eneo la Ludete Katoro washtakiwa walimuua Mawazo kwa kukusudia.

Pia Soma

Hukumu mvutano mazishi ya mawazo kesho

Washtakiwa wote wamekana kutenda kosa hilo na kesi imeahirishwa hadi kikao kingine cha mahakama kuu.

Kigogo Chadema auawa kinyama Geita

 

Chanzo: mwananchi.co.tz