Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi kigogo Jamii Forum yakwama

37986 Pic+jamiiforum Kesi kigogo Jamii Forum yakwama

Wed, 23 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kesi ya kuendesha mtandao ambao haujasajiliwa nchini kwa kikoa cha co. tz (Tanzania domain) inayomkabili mkurugenzi mtendaji wa Jamii Media, Maxence Melo na mwenzake Micke William imeshindwa kuendelea na ushahidi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Kesi hiyo ya jinai namba 458 ya mwaka 2016 ilipaswa kuendelea na ushahidi wa shahidi wa saba jana, lakini wakili wa upande wa mashtaka hakuwapo mahakamani.

Wakili wa Serikali, Elizabeth Mkunde alieleza kuwa wakili wa Serikali, Nassoro Katuga hakuwapo, hivyo kuomba tarehe nyingine kwa ajili kuendelea na ushahidi.

Baada ya maelezo hayo, hakimu mkazi mkuu wa Mahakama hiyo, Huruma Shahidi aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 20 itakapoendelea na ushahidi.

Katika kesi hiyo, washtakiwa wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Desemba 9, 2011 na Desemba 13, 2016 katika eneo la Mikocheni wilaya yaKinondoni.

Washtakiwa wanadaiwa kuendesha mtandao usiosajiliwa nchini na kushindwa kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwa kuzuia taarifa binafsi za wateja wao.



Chanzo: mwananchi.co.tz