Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi inayomkabili IGP, Mwanasheria Mkuu wa Serikali yaahirishwa

IGP7 Kesi inayomkabili IGP, Mwanasheria Mkuu wa Serikali yaahirishwa

Tue, 5 Jul 2022 Chanzo: Mwananchi

Kesi ya maombi madogo ya jinai inayowakabili Mwanasheria Mkuu wa Serikali, (AG), Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Kamanda wa Polisi (RPC) na Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD) Dodoma imeahirishwa baada ya washtakiwa hao kutofika mahakamani.

Katika shauri hilo la maombi madogo ya jinai namba 25/2022, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeiomba Mahakama Kuu kutoa amri ya kuachiwa kwa dhamana mratibu wa Uhamasishaji wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), Twaha Mwaipaya.

Akizungumza nje ya mahakama leo Jumanne Julai 5, 2022, Wakili wa upande wa mashtaka, Fredrick Kalonga amedai kuwa Jaji Dk Adam Mambi amefanya busara kuahirisha kesi hiyo hadi zitakapokwenda mahakamani pande zote mbili.

“Hakuna upande wowote kati ya hao wanne waliokuja Mahakamani kwahiyo zikawa ni Busara za Jaji kwamba hatoweza kuendelea na maombi hayo kwasababu upande wa Serikali haupo”amesema

Kalonga amedai licha ya upande wa pili kutofika mahakamani lakini walipewa hati za wito ambazo kila mmoja alisaini kwa wakati wake.

Kwa mujibu wa kalonga kesi hiyo ilifika Mahakamani hapo kwa ajili ya kusikilizwa na imeahirishwa hadi Julai 11, 2022 itakapokuja tena kwa ajili ya usikilizwaji.

ADVERTISEMENT Maombi ya kesi hiyo yamefunguliwa kufuatia kushikiliwa Mwaipaya kwa zaidi ya siku nne.

Chanzo: Mwananchi