Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi inayomkabili Halima Mdee, Hakimu atoa nafasi ya mwisho

72961 Pic+mdee

Mon, 26 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam nchini Tanzania imeutaka upande wa mashtaka kuieleza mahakama kama hawana mashahidi katika kesi ya kutoa lugha chafu dhidi ya Rais wa Tanzania, John Magufuli inayomkabili Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee useme.

Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa Serikali, Sylivia Mitando kudai leo Jumatatu Agosti 26,2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba kuwa shahidi waliokuwa wanamtegemea kutoa ushahidi anaumwa.

"Leo nilijitahidi kuwasiliana na shahidi nilimpata lakini aliniambia hawezi kufika kwa sababu anaumwa hivyo naiomba mahakama hii ipange tarehe nyingine," amedai Mitando

Hakimu Simba amesema kesi hiyo ipo mahakamani hapo tangu Julai 10, 2017 hadi kufikia leo ni miaka miwili na mashahidi waliotoa ushahidi ni watatu hivyo naomba mfunge ushahidi kama wamemaliza.

 

"Natoa nafasi nyingine ya mwisho leteni mashahidi waje kutoa ushahidi hadi sasa waliotoa ushahidi ni watatu tu sipendi ifike Oktoba mwaka huu nataka nilitolee uamuzi,” amesema Simba.

Pia Soma

Shauri hilo limeahirishwa hadi Septemba 4, 2019 litakapokuja kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.

Katika kesi ya msingi inadaiwa kuwa Julai 3, 2017 katika ofisi za makao makuu ya Chadema zilizopo mtaa wa Ufipa wilayani Kinondoni, Mdee alitamka maneno dhidi ya  Rais John Magufuli kuwa,  ‘anaongea hovyo, anatakiwa  afungwe breki,’ kitendo kinachodaiwa kuwa ni kumdhalilisha Rais na kusababisha uvunjifu wa amani.

Chanzo: mwananchi.co.tz