Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi Maofisa wa Polisi Mtwara yaahirishwa

Screenshot 2022 05 10 At 18.24.40 660x400.png Kesi Maofisa wa Polisi Mtwara yaahirishwa

Tue, 10 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kesi ya mauaji inayowakabili maofisa saba wa Jeshi la Polisi mkoani Mtwara, leo imeahirishwa mpaka Mei 23 mwaka huu.

Kesi hiyo ipo chini ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mtwara, Lugano Kasebele.

Maofisa hao saba, wamefikishwa mahakamani hapo kwa tuhuma za kufanya mauaji ya mfanyabiashara wa madini, Mussa Hamisi (25), mkazi wa Kijiji cha Ruponda wilayani Nachingwea mkoani Lindi.

Kesi hiyo leo ilipangwa kutajwa kwa njia ya mtandao majira ya saa tano asubuhi, lakini kutokana na changamoto ya kimtandao hasa sauti kutosikka vizuri, ikalazimika washitakiwa kufuatwa mahabusu na kufikishwa mahakamani mchana, ndipo ikatajwa na kuahirishwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live