Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi Malinzi yapigwa kalenda

11797 Kesi+pic TanzaniaWeb

Thu, 19 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. kesi ya kughushi na kutakatisha fedha, inayomkabili  aliyekuwa rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini( TFF),Jamal Emil Malinzi(57) na wenzake, imeahirishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Kesi hiyo ambayo ilipaswa jana kuendelea na ushahidi, imeshindwa kuendelea, baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Shadrack Kimaro kuieleza mahakama hiyo kuwa anaomba muda alipitia jalada kabla ya kuendelea na ushahidi, kutokana na shauri hilo kuendeshwa na wakili mwingine.

Kimaro alieleza hayo jana  mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Wilbard Mashauri, wakati shauri hilo lilipokuja kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.

Wakili huyo alidai kuwa, awali shauri hilo, ilikuwa linaendeshwa na Wakili kutoka  Takukuru, Leonard Swai ambaye jana hakuwepo  mahakamani, hivyo wanaomba muda ili aweze kulipitia na kujua walipofikia kwa upande wa mashahidi

" Shauri hili limekuja kwa ajili ya kuendelea na ushahidi, lakini kwa bahati mbaya mimi sikuwepo mahakamani wakati shauri hili linaendelea na ushahidi, hivyo naomba muda wa kuliangalia na kulipitia jalada ili kujua lilipoishia" alidai Kimaro.

Kimaro alidai kuwa hakuwepo  mahakamani kwa muda kutokana na kupata matatizo yaliyomlazimu kusafiri kwenda Moshi, hivyo hajapata fursa ya kulipitia jalada ili ajue limefikia wapi.

"Naiomba mahakama iahirishe shauri hili, ili ipate muda wa kulipitia na kujua walipoishia ili tuendelee na kusikiliza ushahidi kwa sababu, lengo letu ni kuhakikisha kuwa kesi zinasikilizwa na kuisha kwa wakati" alidai Kimaro.

Pia Wakili Kimaro, alidai kuwa upande wa mashtaka walikuwa na shahidi ambaye ni Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidau(41), aliyepaswa kuendelea na ushahidi.

Baada ya Maelezo ya upande wa mashtaka, wakili wa utetezi Richard Rweyongeza, akisaidiana na Nehemiah Nkoko, Kashindye Thabith, Wabeya Kung'e,  Abraham Senguji,  alidia kuwa hawana pingamizi juu ya Maelezo yaliyotolewa na upande wa mashtaka.

Hakimu Mashauri baada ya kusikiliza hoja za pande zote, aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti mosi mwaka huu, itakapoendelea na usikilizwaji.

Tayari mashahidi zaidi ya watano wa upande wa upande wa mashtaka wameshatoa ushahidi wao dhidi ya washtakiwa hao.

Mbali na Malinzi, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa  Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Joas Selestine(46) na Mhasibu wa TFF,  Nsiande Isawayo Mwanga(27).

Wengine ni Meneja wa  Ofisi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),Miriam Zayumba na Karani wa TFF, Flora Rauya ambao Kwa pamoja  wanakabiliwa na mashtaka 30 katika   kesi ya jinai namba 213 ya mwaka 2017 yakiwamo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha wa USD 173,335 na Sh 43,100,000.

Malinzi, Mwesigwa na Nsiande wapo rumande kwa kukabiliwa na utakatishajkuwa katik fedhaambayo kwa mujibu wa sheria hayana dhamana huku wenzao Zayumba na Frola wapo nje kwa dhamana.

Moja ya ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) Dk Paul Marealle  (57), ulieleza kuwa

katika kikao cha kamati tendaji cha Juni 5,2016 hakuwa na ajenda wala barua ya kubadili watia saini katika kikao hicho.

Dk Marealle ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya Tiba ya Shirikisho la Mpira Afrika (CAF) na Daktari Mwandamizi wa Mifupa kutoka Hospitality ya Taifa ya Muhimbili, Kitengo cha Mifupa (MOI), alidai kuwa amekuwa Mjumbe wa TTF tangu  mwaka 2011.

Alidai kuwa Juni 5,2016 alikuwa katika kikao  cha kamati ya utendaji ya TFF, ambacho kilifanyika katika Ofisi za shirikisho hilo, zilizopo wilaya ya Ilala.

Alieleza kuwa kiongozi wa kikao hicho alikuwa ni raisi wa TFF ambaye ni Jamal Malinzi na kwamba kulikuwa na ajaenda 12 zilizojadiliwa ikiwemo  masuala ya michezo na uundwaji wa kamati.

Chanzo: mwananchi.co.tz