Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi 105 udhalilishaji wa kijinsia zafutwa

D6fe32cbf5a55866991606991b491f4d Kesi hizo zimefutwa katika mahakama za Unguja na Pemba

Tue, 24 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kesi 105 za udhalilishaji wa kijinsia zimefutwa katika mahakama za Unguja na Pemba kutokana na kukosekana ushahidi, huku wananchi wakishindwa kutoa ushirikiano wa kuwatia hatiani watuhumiwa wa kesi hizo.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora, Haroun Ali Suleiman wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Pandani, Professa Omar Faki Hamadi aliyetaka kujua kwa nini kesi za udhalilishaji wa kijinsia zimekuwa na kasi ndogo katika kusikilizwa na kutolewa hukumu.

Suleiman alisema kesi 194 za ubakaji zimetolewa hukumu na 57 washtakiwa wake walitiwa hatiani na kuhukumiwa hukumu mbalimbali.

Alisema kesi 460 zinaendelea kusikilizwa katika Mahakama Kuu Unguja na Pemba, lakini changamoto ni wananchi wahusika hawapo tayari kutoa ushahidi mahakamani.

“Changamoto kubwa ya kesi za udhalilishaji ikiwamo za ubakaji ni kwa wahusika wenyewe kukataa kutoa ushahidi mahakamani na matokeo yake hulazimika kufutwa,'' alisema.

Hata hivyo, Suleiman alisema vyombo vinavyosimamia sheria likiwamo Jeshi la Polisi, mahakama na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka (DPP) vimekubaliana kuhakikisha kesi za udhalilishaji zinasikilizwa na kutolewa hukumu katika kipindi kifupi.

“Kesi kuchelewa kutolewa hukumu mahakamani kwa kiasi kikubwa imekuwa changamoto na sababu kubwa ni wananchi wengi kushindwa kutoa ushahidi,” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live