Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kauli, amri za watendaji nchini Tanzania zaibua mijadala

71713 Pic+kauli

Fri, 16 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi/Mwanza. Picha za video na taarifa zinazozunguka katika mitandao ya kijamii zikiwaonyesha watendaji wa Serikali na taasisi zake wakitoa amri na kauli zinazokiuka sheria na katiba zimeibua mjadala.

Mojawapo ni video inayosambaa kwa kasi katika mitandao kuanzia juzi ikimuonyesha mjumbe wa NEC ya CCM Mkoa wa Pwani, Haji Abuu Jumaa akimshurutisha ofisa wa Polisi ambaye jina lake halikujukana mara moja kutoa salaam ya kichama nayo.

Akiwa katika ziara ya kichama katika Kata ya Vianzi, Mkuranga, Jumaa alipokea malalamiko ya wananchi kuhusu kituo cha polisi kutotoa huduma kwa saa 24 kila siku ndipo alipomwita askari huyo kutoa maelezo na kabla ya kufanya hivyo alimtaka kusalimia ki-chama, jambo lililoibua mvutano kati ya wawili hao kama ifuatavyo;-

Jumaa: Hebu salimia kichama kwanza kwani wewe askari wa nani, Chadema?

Polisi: Kawaida askari hanaga chama

Jumaa: Hapana IGP mwenyewe juzi, waziri mwenyewe anatembea na Ilani

Pia Soma

Polisi: Wale ni viongozi

Jumaa: Haya nanihii RPC wa Arusha kaingia kwenye utekelezaji wa ilani ya CCM

Polisi: Wao wanaruhusiwa mimi bado askari mdogo sana

Jumaa: Kwani si salamu tu. Kwani wewe unapata mshahara wa chama gani

Polisi: Nalipwa na Serikali

Jumaa: Serikali gani

Polisi: Ya Mapinduzi. Kiutaratibu askari hatakiwi (akakatishwa)

Tukio hilo limeibua mjadala hasa kutokana na wachangiaji kurejea video nyingine za maofisa wawili waandamizi wa Polisi, wakishiriki vikao vya CCM na kusalimia ki-CCM.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa alisema japokuwa video inasema ni askari aliyehusika anatoka mkoa mwake, yuko Mkoa wa Kipolisi Kibiti Rufiji.

Kwa habari zaidi soma gazeti la Mwananchi la leo Ijumaa Agosti 16, 2019

Chanzo: mwananchi.co.tz