Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Katibu wa CCM Kunduchi kusomewa maelezo ya awali

60546 Ccm+pic

Thu, 30 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni imepanga Juni 26, 2019 kuwasomea maelezo ya awali katibu wa CCM kata ya Kunduchi, Rashid Mchongea  na mfanyabiashara, Rose Mtuli baada ya upelelezi wa kesi inayowakabili ya kuomba na kupokea rushwa kukamilika.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kuomba na kupokea rushwa ya Sh500,000.

Akizungumza mahakamani hapo leo Alhamisi Mei 30, 2019 wakili wa Serikali, Abudi Yusuph amedai mbele ya hakimu mfawidhi, Frank Moshi kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuomba tarehe kwa ajili ya kuwasomea maelezo ya awali.

Baada ya maelezo hayo hakimu Moshi ameahirisha shauri hilo hadi Juni 26,2019.

Wanadaiwa kati ya Agosti Mosi na 15, 2018 Kunduchi, Mchongea aliomba hongo ya Sh500,000 kwa Rose kumshawishi ampunguzie kodi ya pango.

Katika shtaka la pili imeelezwa kuwa kati ya Agosti 15, 2018 katika eneo la Kunduchi, Mchongea alipokea hongo ya Sh500,000 kama kishawishi ili ampunguzie kodi ya pango.

Pia Soma

Katika shtaka la tatu,  kati ya Agosti 15, 2018 eneo la Kunduchi, Rose alitoa rushwa  kwa Mchongea ili apunguziwe kodi ya pango.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz