Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Katibu wa CCM Hai akamatwa na polisi

37710 Polisipic Katibu wa CCM Hai akamatwa na polisi

Tue, 22 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Hai. Katibu wa CCM wilaya ya Hai, Laurence Kumotola, amekamatwa na polisi kwa tuhuma ya kuwazuia askari kufanya kazi yao ya ulinzi, wakati wakitaka kuingia katika ofisi za halmashauri ya wilaya ya Hai.

Tukio hilo limetokea leo majira ya saa 5:45 asubuhi, wakati katibu huyo akiwa ameambatana na wafuasi wa chama hicho pamoja na viongozi mbalimbali, walipodaiwa kuvamia ofisi ya mkuu wa wilaya kwa maandamano na kuzuia watu kuingia katika ofisi hizo hadi wao watakaporuhusiwa na kusikilizwa na mkuu wa wilaya hiyo, Lengai Ole Sabaya.

Katibu huyo akiwa na wafuasi hao, walitumia zaidi ya dakika 10 wakiwa katika geti la kuingia katika ofisi hizo, hadi pale mkuu wa wilaya ya Hai alipotoka na kuruhusu wafunguliwe awasikilize.

Wakati mkuu huyo wa wilaya akizungumza na watu hao, ndipo mkuu wa polisi wilaya ya Hai, Lwelwe Mpina alipoingia na kumwambia mkuu wa wilaya kuwa anamkamata katibu wa CCM kwa kuwa amemzuia kufanya kazi yake.

"Mkuu naomba kumchukua katibu, amenizuia kuingia hapa wakati mimi ndiye nasimamia ulinzi na usalama hapa," alisema OCD.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz