Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Katibu kata CCM matatani

95314 Katibu+pic Katibu kata CCM matatani

Tue, 11 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Sengerema. Zaidi ya Sh600,000 zilizotengwa kwa ajili ya malipo ya ankara ya maji katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Nyampulukano, wilayani Sengerema zimezua jambo baada ya katibu wa kata hiyo kusimamishwa kazi akidaiwa kuzitafuna.

Hata hivyo, katibu huyo, Antony Busumabu amekana kutumia fedha hizo kwa shughuli binafsi, badala yake ameiambia Mwananchi kuwa zilitumika kwenye vikao vya kimkakati vya kuikomboa kata hiyo kutoka mikononi mwa Chadema.

“Tuhuma zinatokana na makundi ya kisiasa kwa sababu viongozi wanafahamu fedha zile zilitumika kurejesha udiwani kata ya Nyampulikano,” alisema.

Mwenyekiti wa CCM Kata ya Nyampulukano, Lugega Festo alidai katibu hiyo alikiri kutumia fedha hizo na aliahidi kuzirejesha.

Chanzo: mwananchi.co.tz