Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Katekista atuhumiwa kubaka mwanafunzi

Katekista Pic Data Katekista atuhumiwa kubaka mwanafunzi

Tue, 24 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simon Njavike (43) ambaye ni Katekista wa Kanisa la Roman Catholic Parokia ya Mlangali Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya hiyo akituhumiwa kwa kosa la kumbaka Mwanafunzi wa kidato cha tatu mwenye umri wa miaka 17.

Mwendesha mashtaka Angelo Marco mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Ludewa Isaac Ayengo amesema Mshtakiwa Simon Njavike ambaye ni Mwalimu wa Watoto wa kipaimara akiwemo Binti huyo amekuwa akifanya vizuri katika mafunzo yake ya Kipaimara hivyo katekista alimpa Tsh. 10,000 kama zawadi ya kufanya vizuri kwenye mafunzo hayo.

Baada ya siku kadhaa Mshtakiwa alianza kumtaka kimapenzi lakini Binti huyo alikataa ndipo akaanza kudai kurudishiwa TSh. 10,000 yake aliyokuwa amempa lakini Binti alishindwa kuirudisha kutokana na kutokuwa nayo.

Ameeleza kuwa baada ya siku kadhaa Mtuhumiwa alimuita Binti nyuma ya kanisa majira ya mchana ambako kuna msitu na binti alipofika akamkamata kwa nguvu na kuingia nae katika msitu kisha akatimiza lengo lake na kutokomea kusiko julikana.

Polisi walifanya jitihada za kumtafuta na baada ya siku kadhaa alikamatwa na kufikishwa Mahakamani ambapo amekana shitaka hilo na kupelekea kesi hiyo kuahirishwa mpaka February 09 mwaka huu

Chanzo: www.tanzaniaweb.live