Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Katavi yaanza kusikiliza kesi 24 za mauaji

Kesipic Data Katavi yaanza kusikiliza kesi 24 za mauaji

Mon, 21 Feb 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Jaji Mfawidhi Kanda ya Sumbawanga, Dunstan Ndunguru ameanza kusikiliza kesi za mauaji 24 katika Mahakama ya hakimu Mkazi mkoa wa Katavi.

Akizungumza baada ya uzinduzi wa usikilizwaji wa kesi hizo uliofanyika leo, Februari 21,2022 Kaimu Naibu Msajili Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga,  Gway Sumaye amesema kesi hizo zitasikilizwa kwa muda wa mwezi mmoja.

“Kwenye kesi hizo 24  mashahidi wanaotakiwa kuitwa mahakamani ni 86 lakini kwa mujibu wa samasi tulizosambaza waliopatikana ni 42,”amesema Sumaye akaongeza.

“Mashahidi 28 bado wanatafutwa,10 wamepigiwa simu wapo tayari kufika tarehe za kesi, samasi 6 zimerudishwa  wahusika walihama katika maeneo yao tunaendelea kuwatafuta"

Amesema kesi ya kwanza ya mauaji ambayo iliyoanza kusikilizwa leo ni ya mshtakiwa Joseph Shigembe dhidi ya Jamhuri na kwamba ina mashahidi 10.

“Upande wa watetezi  kuna mtu mmoja mshtakiwa pekee na kuna wakili Lawrance John anawatetea,”

Chanzo: www.mwananchi.co.tz