Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Karani wa mahakama kizimbani kwa rushwa

85975 Pic+karani Karani wa mahakama kizimbani kwa rushwa

Thu, 28 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Karani wa mahakama ya Wilaya ya Temeke, Itialy Omary amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kosa la kuomba na kupokea rushwa ya Sh200, 000.

Kabla ya kufikishwa mahakamani mshtakiwa alifunguliwa mashtaka pamoja na askari polisi ambaye ni mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke, Leslie Koini aliyekiri kosa la kupokea rushwa ya Sh200, 000 na kuhukumiwa kulipa faini ya Sh700,000 au kwenda jela miaka mitatu.

Akisoma hati ya mashtaka leo Jumanne Novemba 26, 2019 mwendesha mashtaka wa Takukuru, Odessa Horombe amedai Aprili 27, 2018 maeneo ya mahakama ya wilaya ya Temeke mshtakiwa huyo akiwa mahakamani aliomba rushwa ya Sh200, 000 kutoka kwa Musa Abdallah.

Amesema aliomba kiasi hicho cha fedha ili kumsaidia mhusika kukwepa hatia shtaka linalomkabili katika kesi namba 211/2018 ya usalama barabarani.

Amedai Mei 8, 2018,  Koini na Omary walipokea rushwa ya Sh200, 000 kwa Musa Abdallah kama kishawishi cha kumsaidia kukwepa hatia kwenye kesi ya usalama barabarani namba 211/2018 iliyopo katika mahakama hiyo.

Baada ya kusomewa shtaka linalomkabili mshtakiwa huyo alikana na upelelezi umekamilika, Horombe aliiomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali.

">Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 28, 2019. Mshtakiwa yupo nje kwa dhamana.

Chanzo: mwananchi.co.tz