Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampuni inayojenga reli ya SGR yajitenga na makosa ya meneja wake aliyehukumiwa Kisutu

98044 Sgr+pic Kampuni inayojenga reli ya SGR yajitenga na makosa ya meneja wake aliyehukumiwa Kisutu

Fri, 6 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Saalam. Kampuni ya Yapi Merkezi ya Uturuki ambayo inajenga reli ya kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro, imesema haihusiki na makosa ya mfanyakazi wake Mehmet Yetkin Genc aliyekamatwa uwanja wa ndege kwa kushindwa kuzitolea maelezo dola 84,850 alizokutwa nazo wakati akitaka kwenda nje ya nchi.

Mfanyakazi huyo alifikishwa mahakamani na kukutwa na hatia ya kushindwa kutolea maelezo fedha hizo ambazo ni sawa na Zaidi ya Sh170 milioni za Kitanzania zilizokuwa ndani ya begi akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA).

Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu ilimuhukumu raia huyo wa Uturuki kifungo cha miaka mitatu jela, au kulipa faini ya Sh100 milioni na pia kutaifisha fedha hizo alizokutwa nazo.

Taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo katika Gazeti la Mwananchi imesema “imepokea taarifa ya mfanyakazi wake, Mehmet Yetkin Genc ambaye Mahakama ya Tanzania imemuamuru kulipa faini ya Shilingi milioni 100 baada ya kukutwa na hatia ya kushindwa kutolea maelezo ya dola 86,850 zilizokuwa katika begi lake katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA)’.

“Kukutwa na kiwango hicho cha fedha ni kinyume na Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” inasema taarifa hiyo.

“Tunafahamu kwamba Mehmet Yetkin Gene alikiri kosa mbele ya Mahakama, tarehe 13 Februari, 2020, hata hivyo licha ya kukiri kosa hilo ambalo alilifanya wakati akiwa katika safari zake binafsi, kampuni ya Yapi Merkezi isihusishwe na wala haihusiki na makosa hayo.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement
 “Kampuni ya Yapi Merkezi inakemea vikali ukiukwaji wa sheria uliofanywa na Mehmet na pia ni kinyume na kanuni za maadili ya kampuni ambayo inahimiza kuheshimu sheria za nchi ambazo inafanya kazi na ambazo zinatakiwa kufuatwa na kila mfanyakazi. Hivyo tunautaarifu umma kuwa tunatuchukua hatua za kinidhamu kwa mfanyakazi yeyote ambaye atakiuka kanuni na taratibu za kampuni”.

Yapi Merkezi imesema ni nia yao kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli katika kujenga miradi mikubwa ya maendeleo kwa wananchi.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz