Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamchape, Lambalamba njooni mjisalimishe – Mutafungwa

RPC Mutafungwa 1024x640 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Wilbrod Mutafungwa

Sun, 24 Sep 2023 Chanzo: Dar24

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Wilbrod Mutafungwa amewaonya watu wanaofanya uhalifu ndani ya Ziwa Victoria, ikiwemo vitendo vya Uvuvi haramu na kuahidi kuwa Jeshi la Polisi halitomvumilia mtu yeyote mvunja sheria.

Kamanda Mutafungwa ametoa kauli hiyo Septemba 23, 2023 wakati akitoa elimu ya kuzuia uhalifu kwa wananchi wa Kata ya Bugogwa, Sangabuye, Shibula na Kayenze Wilayani Ilemela, katika mwendelezo wa ziara yake ya kutoa elimu ya kuzuia uhalifu kwa makundi mbalimbali ya jamii.

Amesema, tayari ametangaza wakati mgumu kwa wahalifu wanaopora vyavu za wenzao na mazao ya uvuvi, huku akiahidi kuwachukulia hatua kali za kisheria na kuiomba jamii kutoa ushirikiano katika kutokomeza vitendo hivyo, kwani usalama wa nchi si suala la Polisi pekee.

Katika hatua nyingine Kamanda Mutafungwa amekemea vitendo vya Imani za kishirikina, ikiwemo kundi la Kamchape na Lambalamba huku akiwataka wanaoendesha shughuli hizo kujisalimisha kwa Jeshi la Polisi kabla ya msako.

Chanzo: Dar24