Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamati ya IGP yatua Chato kuchunguza kifo mikononi mwa polisi

MISIMEEE Kamati ya IGP yatua Chato kuchunguza kifo mikononi mwa polisi

Mon, 3 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maofisa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) wamefika kijiji cha Mganza wilayani Chato kuchunguza kifo cha Enos Misalaba (34) mtuhumiwa anayedaiwa kufariki dunia akiwa mikononi mwa polisi.

Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, David Misime amesema hayo katika taarifa kwa waandishi na kueleza timu inaongozwa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).

Misime alisema timu itafanya uchunguzi na kupata majibu ya taharuki iliyojitokeza na kupelekea ndugu kugoma kuzika mwili wa marehemu na wananchi kwenda kuchoma kituo cha polisi cha Kata Mganza wakidai polisi wamehusika.

“Timu ya kwanza imefanya kazi yake, wamekamilisha vizuri, wamekuja timu ambayo wanajua namna ya kufanya hiyo kazi, na nafikiri wataikamilisha wakati wowote, timu ya pili ndio ambao wametumwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi,” alisema

Chanzo: www.tanzaniaweb.live