Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamati ya Amani Pwani yalaani mauji yanayoendelea nchini

Padili.jpeg Padri Benno Kikudo wa Parokia ya Tumbi Kibaha akizungumza wakati wa kikao hicho.

Fri, 18 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamati ya amani ya Mkoa wa Pwani imelaani vikali vitendo vya uvunjifu wa amani vinavyopelekea mauaji kwa watu wasiokuwa na hatia .

Kauli hiyo ya kulaani vitendo hivyo vya kikatili na mauaji ya watu katika jamii ambavyo vimeripotiwa na vyombo mbalimbali nchini Kamati hiyo imesema kuwa hii ni aibu kwa Taifa huku ikisema kuwa wakati Sasa umefika kwa jamii nzima kufanya jitihada za makusudi kyepeuka fedheha hii.

"Jitihada za makusudi zichukuliwe kwa kuanzia katika ngazi ya familia tuanzie chini halafu twende juu kwani katika maisha ya hivi sasa tamaduni zetu zimebadilika kutokana na utandawazi utu wa mtu hakuna Tena, watu hawana hofu ya Mungu Tena hili ni janga hivyo ni wajibu wetu sisi kama.viongozi wa kidini kuungana na kupaza sauti kwani Sasa imetosha" alisema Mwenyekiti Mwenza Kamati ya Amani Mkoa wa Pwani Padri Benno Kikudo wa Kanisa Katoliki Parokia ya Tumbi Kibaha.

Padri Kikudo alisema hayo katika Mkutano Maalumu wa ndani wakati Kamati hiyo ilipozungumza na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaj Abubakari Kunenge huku mkutano huo uliohudhuriwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Pwani mkutano huo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano uliopo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Padri Kikudo alisisitiza kwa kusema kuwa viongozi wa dini wote kwa ujumla wao waungane kwa kutoa mahubiri kwa waamini wao katika Misikiti na Makanisa watoe mahubiri ambayo yatawskumbusha jamii kukijenga kizazi cha sasa kiwe chenye maadili na hofu ya Mungu.

Aidha kauli hiyo iliungwa mkono na na Mwenyekiti Mwenza ambaye pia ni Sheikh Wwa Mkoa wa Pwani Hamisi Mtupa.

Mratibu wa shughuli za Kamati hiyo Mkoa wa Pwani Ibrahim Gama alisema kuendelwa kukithiri kwa vitendo vya mmomonyoko wa maadili Kamati hiyo imeshauri itolewe elimu kwa jamii Ili kumaliza matukio ya mauaji yanayoendelea.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaj Abubakari Kunenge amewashukuru viongozi hao na kwamba atasimia amani na utulivu ndani ya Mkoa wa Pwani huku akiwataka wakaazi wote Mkoani hapa kuwa na mioyo ya Upendo na kusameheana ikiwa ni pamoja na kuacha roho zenye visasi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live