Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamanda asema polisi wana ushahidi wa picha za CCTV kifo cha Mtawa

14690 Mtawa+pic TanzaniaWeb

Thu, 30 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza, Jonathan Shanna amesema picha za kamera za CCTV walizonazo zinamuonyesha aliyekuwa mfanyakazi wa Hospitali ya Bugando, Mtawa Suzan Batholomeo (48) akipanda kwenda ghorofani na kujirusha.

Hivyo ameitaka jamii kuacha kusambaza uzushi kuwa huenda mtawa huyo aliuawa.

Mtawa huyo alifariki akidaiwa kujirusha gorofani Agosti 28 mwaka huu.

Akizungumza leo Agosti 30,  Shanna amesema: “Tuna vithibitisho kamili ikiwamo kamera za CCTV zikimuonyesha Mtawa huyo akipanda ghorofani na wakati akijirusha, hivyo hayo yanayosemwa kwenye mitandao wasiyaamini sana.”

Ameutaka umma kuacha kuamini tetesi za mitandao ya kijamii kuhusu tukio hilo.

Pia, Shanna amesema wanaendelea kufanya uchunguzi na hivi karibuni (hakutaja ni muda gani) ataita vyombo vya habari ili kujibu maswali ya wananchi waliyokuwa wakijiuliza kuhusu kifo cha Mtawa huyo.

Kuhusu mtawa huyo kugawa mali zake kwa ndugu siku chache kabla ya kifo chake, Shanna amesema hawezi kulizungumzia kwa sasa kwani linaweza kuharibu uchunguzi unaoendelea.

Siku chache kabla ya kifo chake, ofisi ya mtawa huyo aliyekuwa mkurugenzi wa fedha ilikuwa akikabiliwa na upotevu wa zaidi ya Sh300 milioni.

Soma Zaidi:

Mtawa ajirusha ghorofani, afariki dunia

Chanzo: mwananchi.co.tz