Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamanda aelezea hatima ya DED Itigi kufikishwa mahakamani

40788 Pic+itigi Kamanda aelezea hatima ya DED Itigi kufikishwa mahakamani

Mon, 11 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Manyoni. Jana ilikuwa siku ya tano tangu Jeshi la Polisi mkoani Singida limkamate mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, Pius Luhende na wenzake sita.

Luhende na wenzake wanatuhumiwa kwa kosa la kumuua kwa kumpiga risasi Isaka Petro (28) wa Kijiji cha Kazikazi kwa kile kinachotajwa ni sababu za madai ya ushuru wa mashamba.

Jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Sweetbert Njewike alisema watuhumiwa wote saba hawajafikishwa mahakamani kutokana na kusubiri taratibu zingine.

“Hatujawapeleka mahakamani bado, kuna taratibu nyingine hazijakamilika, kwa sasa tunaandaa taarifa ya kumpelekea mwendesha mashitaka wa Serikali ambaye ataandaa taratibu za kuwafikisha mahakamani,” alisema Kamanda Njewike.

Februari 2, inadaiwa kuwa Luhende aliongoza kikosi cha watu sita kwenda Kanisa la Wasabato katika Kijiji cha Kazikazi na baada ya kufika, waliwafungia ndani ya kanisa waumini kwa lengo la kuwasaka wakwepa kodi ya mashamba ya Tanganyika Packers kabla ya kumpiga kwa risasi kichwani, Isaka na kufariki dunia hapo hapo.

Waumini wa kanisa hilo pamoja na ndugu wa marehemu walisema kijana huyo alipigwa risasi na Mkurugenzi Luhende lakini baadaye taarifa iliyotolewa na polisi kwa vyombo vya habari ilidai wakati risasi ikipigwa, mkurugenzi huyo alikuwa ameondoka eneo la tukio na wanaodaiwa kumuua kijana huyo kwa risasi ni askari wa wanyamapori waliokuwa kwenye msafara huo wa mkurugenzi.

Kwa maelezo ya waumini hao, kiongozi huyo aliingia ndani ya kanisa akiongozana na mtendaji wa Kijiji na ofisa kilimo wa wilaya na yeye alionekana kumtafuta mtu huku akimuamuru mtendaji amuonyeshe na wakati huo watu wengine walikuwa wakipigwa bila kuelezwa sababu.



Chanzo: mwananchi.co.tz