Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kaka asimulia mstaafu wa Bandari alivyowaaga wafanyakazi wenzake

36855 Mamapic Kaka asimulia mstaafu wa Bandari alivyowaaga wafanyakazi wenzake

Thu, 17 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mamia ya waombolezaji leo Jumatatu Januari 15, 2019 wamejitokeza kuaga mwili wa aliyekuwa mfanyakazi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Tunsume Sakajinga huku kaka wa marehemu akieleza jinsi dada yake alivyowaaga wafanyakazi wenzake.

Tunsume aliuawa Jumamosi iliyopita Januari 12, 2019 saa tano asubuhi kwa kupigwa na kitu kizito kichwani kisha kuchomwa na mkasi ambao uliachwa shingoni mwake.

Mwili wake ulikutwa chini ya sinki la kuoshea vyombo huku ukiwa umefunikwa mkeka na kwa mujibu wa Jeshi la Polisi uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.

Marehemu amesafirishwa leo kuelekea kijiji cha Kasanga Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya kwa ajili ya mazishi.

Leo imefanyika ibada ya mzishi nyumbani kwa marehemu mtaa wa Mgeninani wilayani Temeke.

Kaka wa marehemu, Kissa Mwankusye amesema baada ya dada yake kustaafu Desemba 31, 2018 alienda kazini kuwaaga wafanyakazi wenzake.

“Alisema kuwa watu wakishastaafu maisha yao huwa ni mafupi. Hatujui aliona nini mbele yake hiyo siku ya Alhamisi alipokwenda kuwaaga wenzake. Itoshe tu kumwambia Mungu asante," amesema Mwankusye.

Awali akisoma wasifu wa marehemu, Noah Mwambapa amesema kabla ya kuanza  kazi bandarini mama huyo alikuwa anafanya kazi Shirika la Reli (TRC) "Tunsiime alizaliwa mwaka 1959 na kwa mara ya kwanza aliajiriwa mwaka 1985, amekuwa mtumishi mpaka alipostaafu mwaka jana,” amesema.

 Soma Zaidi: Jinsi mstaafu wa Bandari alivyouawa kwa mkasi Dar



Chanzo: mwananchi.co.tz