Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kajeri atupwa jela miaka sita kwa kosa la kujaribu kubaka

MAHAKA HI 1 Law Atupwa jela miaka sita kwa kosa la kujaribu kubaka

Fri, 29 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

David Juma maarufu kama Kajeri mwenye umri wa miaka 24 mkazi wa Songe  Manispaa ya Musoma mkoani Mara ambaye ni dereva wa pikipiki amehukumiwa kifungo cha miaka 6 jela na kulipa faini ya shilingi Milioni 2.5 kwa kosa la kujaribu kubaka na kudhuru mwili wa binti wa miaka 26

Akisoma hati ya mashitaka mwendesha mashitaka wa serikali Monica Hokororo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Stanley Mwakihaba amesema mshitakiwa david Juma anakabiliwa na kesi ya Jinai no. 41 ya mwaka 2022 ambapo mshitakiwa huyo anakabiliwa na mashitaka mawili shitaka la kwanza la kujeruhi mwili na shitaka la pili ni shambulio la Aibu.

Hokororo ameiambia Mahakama hiyo kuwa mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo tarehe 15 ya mwezi wa 5 ya mwaka huu katika eneo la Nyabange wilaya ya Butiama   alipokodiwa na binti huyo na mshitakiwa huyo ametenda makosa hayo kinyume na vifungu vya sheria ya makosa ya jinai.

Ambapo Kosa la kujeruhi ni kinyume na kifungu cha sheria no.225 sheria ya kanuni ya adhabu sura no. 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2019 na kosa la pili la shambulio la aibu ni kinyume na kifungu cha sheria no.138 D (1) cha kanuni ya adhabu sura no. 16 iliyofanyiwa mapitio mwaka 2019.

Mwendesha mashitaka Hokororo ameiambia mahakama hiyo kuwa david alipokodiwa na binti kuyo kwa ajili ya usafiri lakini alipo fika eneo ambalo linavichaka akaamua kuondoa pikipiki yake barabarani na kuipeleka vichakani kwa lengo la kufanya ubakaji ambapo binti huyo aliamua kuruka kutoka kwenye pikipiki na kuanguka kisha akaanza  kukimbilia barabarani na kupiga kelele za kuomba msaada .

Amesema eneo hilo Halina makazi ya watu hivyo ilimchukua takribani dakika 45 kwa binti huyo kupata msaada ambao ulitoka kwa wasamaria ambao walikuwa wasafiri pamoja na dereva wa gari ndogo baada ya kukuta tukio hilo liketendeka kando kidogo ya barabara na binti akiwanapiga kelele za kuomba msaada.

Hokororo amesema upande wa jamuhuri ulileta mashahidi watatu ambao walitoa ushaidi wao mbele ya mahakama na mtuhumiwa hakuwa na wakili wala shahidi hivyo alijitetea mwenyewe na kusema hakutenda kosa hilo na kuiomba mahakama hiyo kumpunguzia adhabu kwani anamtoto mdogo ambae anamtegemea.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu mkazi mwandamizi Stanley Makihaba amesema mahakama hiyo imemtia hatiani mtuhumiwa huyo pasi kuacha shaka lolote juu ya ushaidi ulio tolewa dhidi yake.

Hakimu Mwakihaba amesema kuwa kulingana na vifungu vya sheria vya makosa ya jinai mtuhumiwa huyo ataenda jela miaka 6 ambapo kila kosa atatumikia kifungo cha miaka mitatu na kulipa faini ya shilingi milioni 2.5 kwa mlalamikaji ambae alivunjika mkono na kupata majeraha mbalimbali ndani ya mwili wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live