Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM Tawi la Sokoni Kata ya Sirari wilayani Tarime mkoani Mara, Moshi Sayi Maduhu, ameuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kifuani karibu na shingoni baada ya kutokea ubishi wa kisiasa kati yake na mfuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Senga Shuri.
Kufuatia hali hiyo, Shauri ambaye ni fundi baiskeli anashikiliwa na Jeshi la Polisi kituo cha Sirari.
Kamanda wa Polisi Tarime Rorya ACP William Mkonda, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema lilitokea Jumamosi 16 jioni katika Kitongoji cha Sokoni wakati wa ugomvi kati ya Maduhu na Shuri aliyekuwa na kisu kisha kumchoma kifuani na kumsababia kifo.
Alisema mtuhumiwa amekamatwa na wanamhoji na baadae atafikishwa kwenye vyombo vya sheria.