Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kabendera asema anaendelea na mazungumzo na DPP

85237 KABDENDERA+PIC Kabendera asema anaendelea na mazungumzo na DPP

Fri, 22 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwandishi wa habari nchini Tanzania, Erick Kabendera ameieleza Mahakama kuwa bado anaendelea na mazungumzo na Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania (DPP).

Ni baada ya kumuandikia barua ya kukiri na kuomba msamaha kwa DPP.

Kabendera anakabiliwa na mashtaka matatu, ambayo ni kuongoza genge la Uhalifu, kukwepa kodi na kutakatisha zaidi ya Sh. 173.2Milioni.

Kupitia wakili wake, Jebra Kambole mshtakiwa huo ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Jumatano Novemba 20, 2019, kuwa bado wanaendelea na mazungumzo.

Amedai bado wanaendelea na mazungumzo na DPP na kwamba wakishafikia makubaliano hayo wataieleza mahakama hiyo.

Kambole aliieleza mahakama hiyo, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Janeth Mtega, wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.

"Mheshimiwa hakimu, mpaka sasa  bado tunaendelea na mazungumzo na DPP, hatujafikia muafaka, tukishafikia makubaliano tutaitaarifu  mahakama" amedai Kambole.

Kambole baada ya kueleza hayo, wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon  amedai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika, hivyo anaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Kuhusu maombi ya mshtakiwa huyo aliyomuandikia DPP, wakili Simon amedai yanafanyiwa kazi na yakikamilika mahakama itapewa taarifa.

Katika hatua nyingine, kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 75/2019 imehamishiwa kwa hakimu Mtega, baada ya hakimu aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo Augustine Rwizile kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.

Hakimu Mtega baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote, amesema kesi hiyo imehamishiwa kwake hivyo atalipitia jalada.

Baada ya kueleza hayo, hakimu Mtega ameahirisha kesi hiyo hadi Desemba 4, 2019 itakapotajwa na mshtakiwa amerudishwa rumande.

Kabendera alifikishwa Kisutu kwa mara ya kwanza, Agosti 5, 2019, wakikabiliwa na mashtaka hayo.

Katika shtaka la kwanza, mshtakiwa anakabiliwa na kosa la kujihusisha na genge la uhalifu.

Alidai katika tarehe tofautitofauti kati ya Januari mwaka 2015 na Julai mwaka 2019, alitenda kosa la kutoa msaada kwa genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia maslahi.

Katika shtaka la pili, Kabendera anadaiwa mshtakiwa anakabiliwa na shtaka la ukwepaji kodi, zaidi ya Sh173.2 milioni.

Kabendera anadaiwa katika tarehe tofauti tofauti kati ya Januari 2015 na Julai 19, 2019, mshtakiwa huyo alishindwa kulipa kodi kiasi cha Sh173.2 milioni.

Chanzo: mwananchi.co.tz