Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#KESIYASABAYA: Uamuzi kukamatwa shahidi kujulikana jumatatu

Sabayaaapicc Leo Uamuzi kukamatwa shahidi kujulikana jumatatu

Fri, 3 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imepanga kutoa uamuzi mdogo iwapo itatoa hati ya kukamatwa kwa shahidi wa 10 wa Jamhuri, Francis Mroso ama la kutokana na ombi la wakili wa utetezi kuwa shahidi huyo akamatwe akidai alitoa rushwa ya Sh90 milioni.

Uamuzi huo mdogo utatolewa Jumatatu (Desemba 6) ambao ulitokana na ombi la wakili wa utetezi, Fridolin Bwemelo katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita.

Juzi, mbele ya Hakimu Mkazi, Patricia Kisinda anayesikiliza kesi hiyo, Wakili Bwemelo, aliiomba Mahakama itoe hati ya kukamatwa kwa shahidi huyo, kwani alikiri kuwa alitoa rushwa hiyo.

Akitoa uamuzi mdogo jana, Hakimu Kisinda aliwapa upande wa Jamhuri muda wa saa mbili wajiandae ili kujibu hoja hiyo badala ya wiki mbili walizoomba wakapate ushauri kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP). Baada ya maelezo hayo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Felix Kwetukia alisema hakuna sababu ya kupewa muda huo na kuwa wanaweza kujibu hoja hizo kwa muda huo.

Akiwasilisha hoja hizo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tarsila Gervas aliieleza sheria imeeleza kuwa DPP anaweza kutoa mamlaka kwa wasaidizi wake, wakiwamo maofisa waandamizi kuendesha mashtaka kwa niaba yake.

“Lakini ili kufanya mamlaka hayo yatekelezwe, sheria zimeonyesha majukumu hayo yanaweza kufanywa na watu wengine, maofisa waandamizi kama mimi ninayeongea mbele ya mahakama hii.

“...kwa upande wangu mawakili wa utetezi wawe wanapitia sheria kabla ya kuleta hoja mahakamani ambazo zinatumalizia muda wa kumaliza shauri hilo badala yake linaleta zogo zisizokuwa za kisheria,” alieleza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live