Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#KESIYASABAYA: Sabaya awakana watuhumiwa wenzake

Sabaya Pic Datadukn Lengai Ole Sabaya, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai

Wed, 19 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Lengai Ole Sabaya ameiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kuwa hawafahamu baadhi ya watuumiwa mwenzake katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili yeye na wenzake sita.

Akitoa Utetezi wake leo, Jumatano, Sabaya amedai kuwa mara yake ya kwanza kuwaona watu hao ni Juni 4, 2021 alipopandishwa kizimbani na kusomewa mashitaka ya uhujumu uchumi.

Watuhumiwa hao ni pamoja na Enock Togolon Mkeni Watson Mwahomange, na John Aweyo Odemba.

Vilevile amedai watuhumiwa wengine wawili Jackson Macha na Nathan Msuya waliletwa katika gereza la Kisongo Juni 21, 2021 ambapo nao walidai ni watuhumiwa wa kesi ile ile ya uhujumu Uchumi inayomkabili Sabaya.

Hata hivyo amebainisha kuwa mtuhumiwa Sylvester Nyegu alikuwa akimuona katika Halmashauri ya Wilaya ya Hai kama mtumishi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live