Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#KESIYASABAYA: Sabaya angua kilio mahakamani

Sabayaapic Data Lengai Ole Sabaya, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai

Wed, 19 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshitakiwa namba moja Lengai Ole Sabaya katika kesi ya uhujumu inayomkabili na wenzake amejikuta akitokwa na Machozi mahakamani hapo wakati akitoa ushahidi wake kama sehemu ya utetezi wake.

Hayo yametokea baada ya wakili wake Mosses Mahuna kumuuliza Sabaya yeye anasemaje kuhusiana na ushahidi wa shahidi wa 13 Ramadhani Rajabu Juma, wa kuiambia mahakama kuwa Sabaya aliunda genge la kihalifu.

Ndipo Sabaya akasema shahidi Ramadhani Juma asifanye kazi ya siasa kwa kumsingizia na kumkandamiza, Sabaya amesema aliweka uhai wake rehani kwa kufanya kazi za serikali,mpaka akatumiwa watu kumuuwa, hivyo basi Ramadhani afanye kazi ya serikali na sio kushirikiana na wafanyabiashara pamoja na mtu aliyedhani amemnyima ubunge kumsema yeye.

Lengai Ole Sabaya akiwa amesimama kizimbani kwa kutaka kuendelea kutoa ushahidi wake juu ya hilo ghafla akawa anatokwa na machozi,na kushindwa kujibu kitendo kilichomfanya akae katika kizimba hicho na kujiinamia chini huku akitokwa na machozi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live