Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#KESIYASABAYA: Sabaya aanza kujitetea kesi ya Uhujumu Uchumi

Cctv Sabaya Sabaya aanza kujitetea kesi ya Uhujumu Uchumi

Wed, 19 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshtakiwa Lengai ole Sabaya anyekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi amepanda kizimbani kutoa utetezi dhidi ya tuhuma hizo ambapo amewakana mashahidi wa jamhuri na kudai mashtaka hayo ni ya kutungwa.

Akitoa utetezi wake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha leo, Jumanne, Sabaya amedai hamfahamu Mfanyabiashara Fransis Mroso wala Adam Best ama Peter Marandu ambao aliwaona mahakamani wakitoa ushahidi.

Katika kesi ya Uchumi, inadaiwa Sabaya na wenzake walichukua rushwa ya Sh milioni 90 kutoka kwa Mfanyabiashara Mroso na baadaye Sabaya aligawa kiasi cha fedha hizo na nyingine kujinunulia gari aina ya Toyota V8 kutoka kwa mfanyabiashara mwingine jijini Dar es Salaam.

Sabaya alijitetea kwamba ushahidi uliotolewa mahakamani hapo hauna ukweli wowote. Amedai, Shahidi wa 13, Ramadhani Juma ambaye awali alifahamika kama afisa uchunguzi wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ni mtaalamu wa maendeleo ya jamii na kwamba hana uwezo wa kuchambua taarifa za mtandao wa vodacom.

Sabaya amesema wakati simu zake zilizofanyiwa uchunguzi ziko Takukuru, mnara unaonesha Sabaya yuko Kisongo Gerezani.

Vilevile, Sabaya amedai kuwa siku ya tukio, Jan. 22, 2021 ilidaiwa kuwa yeye pamoja na dreva akitumia gari ya serikali STL5434 alikuwa katika maeneo tofauti tofauti ya Arusha wakati ukweli alikuwa kazini Boma Ng’ombe Hai na baada ya kazi alirejea nyumbani kwakwe na hakutoka.

Sabaya anayetumikia kifungo cha miaka 30 jela kwa kufanya unyang’anyi wa kutumia silaha amesisitiza kuwa taratibu za utumishi ziko wazi na kwamba yeye pamoja na dreva wasingeweza kuondoka katika eneo lao la kazi bila kutoa taarifa kwa Katibu Tawala wa Wilaya na yule wa Mkoa.

Aliongeza pia kuwa yeye hakukamatwa na Maafisa wa Takukuru akiwa hotelini kama walivyo eleza katika ushahidi bali walimkamata akiwa chumbani kwake yeye na mke wake baada ya kumvamia na kupita dirishani.

Kesi hii inaendelea kusikilizwa kesho, Jumatano na endelea kufuatilia ukurasa wetu na tovuti kwa ajili ya kufahamu kitakachokuwa kikiendelea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live